Ngeli ni neno linalotumiwa kuelezea upangaji wa nomino za Kiswahili kwa kuzingatia sifa zinazofanana. Sifa hizi zinaweza kuwa za kimaana, kimuundo na hata kisarufi. Ngeli ni vikundi vya maneno yenye sifa sawa na bainifu ambavyo nomino hupangwa. Aidha, ngeli huweza kuelezwa kama utaratibu wa kuzipanga nomino za Kiswahili kulingana na upatanisho wa kisarufi. Hapa, huwa tunapata ngeli za Kiswahili kwa kutumia kiambishi tamati cha kivumishi kiashiria cha karibu au kiambishi awali cha kwanza cha kitenzi katika umoja na wingi.
Kwa kuzingatia uupangaji wa nomino za kiswahili kwa kuzingatia sifa zinazofanana tunapata ngeli zifuatazo:
- Ngeli ya A-WA
- Ngeli ya U-I
- Ngeli ya U-ZI
- Ngeli ya YA-YA
- Ngeli ya I-I
- Ngeli ya U-U
- Ngeli ya LI-YA
- Ngeli ya U-YA
- Ngeli ya KI-VI
- Ngeli ya KU-KU
- Ngeli ya I-ZI
- Ngeli ya PA-KU-MU
- Ngeli ya ZI
- Ngeli ya VI
- Ngeli ya LI
- Ngeli ya A