Sababu za fasihi simulizi kuwa sanaa

Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu.
Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha fikra na hisia za binadamu kama vile maneno, maandishi,
uchoraji, uchongaji, ufinyanzi n.k.
Fasihi simulizi ni sanaa kwa vile:
a) Huwasilisha ujumbe kuhusu binadamu kuhusu utamaduni na uchumi.
b) Huwa na umbo mahsusi k.m. hadithi huwa na mwanzo, kati na mwisho na mashairi
huwa na beti, mishororo, n.k.
c) Hutumia lugha kwa ufundi k.v. ya kitamathali.
d) Husawiri mandhari/mazingira mahsusi kwa ufundi mkubwa.
e) Hujenga wahusika kwa ustadi mkuu ili kusawiri tabia za watu katika jamii.

Leave a Reply

scroll to top