SABABU ZA KUCHUNGUZA SIFA BAINIFU/ PAMBANUZI

 

1.      Kujumuisha vitamkwa vinavyochangia sifa fulani.

2.      Kutenga makundi asilia yanayochangia mahali pa matamshi n.k. mfano, vitamkwa vya msingi vinaweza kuwekwa katika makundi asilia.

3.      Waliona kuwa kuna sifa zitumikazo katika kila lugha duniani, mfano, sifa ya ukonsonanti [+konso]. Nayo huhusisha vitamnkwa vinavyohusishwa msuguano katika utokeaji wake ambao waweza kuwa wa kubana, mwembamba au wa kimadende. Hali hii huletelea makundi kama ya: vizuio, vikwamizi, ving’ong’o, vitambaza na vimadende. Waliona pia kuna uwepo wa usilabi [+sil]. Ving’ong’o, vitambaza huwa na usilabi katika baadhi ya lugha. Waliona kwamba ni vema wabague/ watenganishe kati ya ving’ong’o na vitambaza/ vimadende.

► Sifa ya Usonoranti

Kuna ughuna wa vitamkwa kama vile vyenye usilabi na hakuna mguno kwani mkondohewa hauzuiliwi. Ukonsonanti, usilabi na usonoranti huweza kuletelea aina mbalimbali ya makundi. Vipasuo ndani, vikwamizi kwani kuna vitamkwa vina sifa ya ukonsonanti na hazina usonoranti wala usilabi.

hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top