Sauti

Sauti  ni mlio unaotoka kwa ala za kutamkia kinywani. Au   kipashio kidogo zaidi katika lugha ambacho hakina maana kisarufi. mfano wa sauti ni kama vile

/b/, /n/,/a/ ,/e/, /m/, /k/, /f/,/d/ n.k

Tanabahi: Ni muhimu kukumbuka kuwa unapoandika sauti ni lazima ziandikwe kwa herufi ndogo na  mzashari au mkwaju kutumika. 

ikiwa tutachukua sauti /k/ na sauti /a/ na kisha kuziunga pamoja tunatengeneza silabi ka na silabi hii tukiunga pamoja na silabi nyingine tunaunda neno kaka na kisha tukiunga maneno pamoja tunaunda kipashio kikubwa zaidi ambacho ni sentensi.

kwa mfano;

Kaka ameenda shuleni. Hii ni sentensi ambayo imeundwa kwa maneno matatu

Kaka – nomino

ameenda – kitenzi

shuleni – kielezi

Leave a Reply

scroll to top