Semi- Koloni (;)

Semi – koloni au Nukta- mkato huwa na matumizi mbalimbali kama ifuatavyo:

  1. Huashiria mtuo au kupumzika fulani katika sentensi ambayo ni ndefu. Kwa mfano: Kila nitembeapo barabarani na marafiki, mimi huwaza kuhusu mbinu mwafaka za kufaulu masomoni; nimekuwa nikijitahidi sana masomoni ila alama zangu hazijaimarika.
  2. Kuunganisha sentensi mbili au vishazi viwili ambavyo haviwezi kusimama huru bila kuwako kiungo fulani. Kwa mfano: Mwaka huu tumeshuhudia mvua kubwa maeneo haya ya mashariki ya nji; ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita ambapo kumekuwa na kiangazi zaidi.
  3. Katika sentensi ambatano hasa pale ambapo viunganishi na, lakini, au n.k. vimeachwa na havitumiki. Mfano katika sentensi: Amendika jana Jioni; atarudi huku kesho asubuhi.
  4. Hutumiwa kabla ya maneno kama ‘hata hivyo’ na ‘vinginevyo’ yanapotumiwa kuunganisha vishazi huru viwili. Kwa mfano: Wanafunzi wa sayansi ni wavivu sana; hata hivyo, wamejibidiisha sana kusoma muhula huu.
  5. Hutumiwa kabla ya maneno ya kutolea maelezo ya ufafanuzi kama yaani, kwa mfano, katika sentensi: Kuna sababu nyingi za kuwa na maandano nchini dhidi ya serikali; kwa mfano, Ufisadi, mauaji ya alahiki shakahola,gharama ya juu ya maisha, mfumko wa kiuchumi, na bei ghali ya mafuta.
  6. Hutumika katika sentensi ambapo kuna orodha na koma zinazotokea katika orodha hiyo. Kwa mfano: Kuna ina mbali mbali za nyimbo kama hodiya; nyimbo za jadiya;tahalili;nyimbo za kisasa na tumbuizo.
ALAMA ZA UAKIFISHA
Alama za usemi(“”)
Dukuduku (…)
Koma/mkato/kipumuo( , )
Ritifaa/kibainishi( ’ )
Mshazari/mkwaju(/)
Kistari kifupi( – )
Kistari kirefu
Mstari( ___  )
Kikomo/kitone/nukta (.)
Vifungo/mabano/paradesi( )
Herufi kubwa(H)
Herufi ndogo (h)
Koloni/ Nukta mbili ( : )
Hisi/mshangao (!)
Herufi nzito (h)
Herufi za mlazo/italiki(h)
Kinyota(*)
Swali/Kiulizo

Leave a Reply

scroll to top