Kiimbo

Kiimbo ni jinsi sauti inavyopanda na kushuka mtu anapoongea.

Umuhimu wa kiimbo:

 i) Husaidia katika utamkaji sahihi wa  maneno  au sentensi na hivyo kudhihirisha maana iliyo kusudiwa na msemaji

ii) Huonyesha hisia zinazojitokeza  katika usemi wa mtu kama vile hasira, swali na kadhalika.

baadhi ya maneno hubadilisha maana  kutegemea na sehemu ya sauti iliyotiliwa mkazo

Kutokana na kiimbo sentensi huwa na uamilifu/majukumu(functions) zifuatazo:

Uamilifu wa sentensiMfano
Sentensi za taarifaGari limeanguka.
Sentensi za maswaliGari limeanguka?
Sentensi za mshangao Gari limeanguka!
Sentensi za amriKachezeeni nje!
Sentensi za rai/ombiNisaidie/eni.

        Zoezi

  1. Eleza maana ya kiimbo kwa kutoa mifano.
  2. Tambua sentensi zifuatazo ni za aina gani kutokana na kiimbo.
    1. Watu wanakula nyoka?
    2. Watu wanakula nyoka.
    3. Watu wanakula nyoka.
    4. Tafadhali nisaidie.

Shadda/Mkazo

Shadda ni mkazo unaowekwa kwenye silabi  ya neno linapotamkwa ili kutoa maana iliyo kusudiwa.Sauti zinazotiliwa nguvu zaidi husikika vizuri kwani hutokea kwa nguvu zaidi,ilhali nyingine katika neno ambazo hatiliwi nguvu huwa hafifu. Alama ya ritifaa hutumiwa kutambulisha shadda.Huwekwa kwenye silabi ya pili kutoka mwisho wa neno.

Umuhimu wa Shadda

  1. Mkazo hutumiwa kutofautisha maana za maneno tofauti.

Kwa mfano neno bara’bara likiwa na maana ya njia/baraste na ba’rabara likiwa na maana ya vyema/vizuri na wala’kini (lakini), wa’lakini (kasoro/dosari/ila)

  1. Shadda  huchangia matamshi bora.

Zoezi

  1. Weka shadda katika maneno haya:
  1. imba
  2. baba
  3. Onyesha kwa kupiga mstari iliko shada katika maneno yafuatayo:
  1. malaika
  2. nge