Shamirisho ala /kitumizi.
Huonyesha kile ambacho husaidia kutendeka kwa jambo au kitendo fulani katika sentensi.Ni kifaa ambacho hutumika, Mfano :
Mama anampikia mtoto chakula kwa sufuria, Kibarua alimlimia mkulima shamba kwa jembe.
Katika sentensi hizi mbili, sufuria na jembe ni Shamirisho ala au kitumizi.
Mifano Zaidi
- Mama alimpikia baba chakula kwa sufuria.
- Baba alipikiwa chakula na mama kwa sufuria.
- Sufuria ilitumiwa na mama kumpikia baba chakula.
- Chakula (Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa)
- Baba (Shamirisho Kitondo/Yambwa atendewa)
- Sufuria (Shamirisho Ala/Yambwa Kitumizi)
Shamirisho |
Shamirisho kipozi /yambwa tendwa. ( direct object) |
Shamirisho kitondo /Yambwa tendewa. (indirect object) |