Shamirisho kipozi /yambwa tendwa. ( direct object)
Huonyesha kile kinachotendwa katika sentensi; Huonyesha kile ambacho hupokea athari ya kitenzi moja kwa moja. Mfano:Mpishi anapika chakula , Mwanafunzi anaandika kitabu .
Katika sentensi hizi mbili, chakula na kitabu ni kipozi/ yambwa tendwa
Mifano zaidi:
Nyumba kubwa iliyojengwa jana imebomoka.
Anita alimkatia mtoto mkate kwa kisu.
Mwanaheri alinunua simu yenye rangi nyingi.