Shamirisho kitondo

Shamirisho kitondo /Yambwa tendewa. (indirect object)

Ni nomino ambayo huathiriwa na kitendo kwa njia isiyo ya moja kwa moja.Sentensi nyingi huwa na vitenzi katika kauli ya kutendea/kutendewa. Yambwa tendewa huwa ni nomini inayofaidi kutokana na kitendo Huonyesha kile ambacho hupokezewa athari ya kitenzi katika sentensi. Mfano :Mama anampikia mtoto chakula, Kibarua alimlimia mkulima shamba.Katika sentensi hizi mbili, mtoto na mkulima ni kitondo au yambwa tendewa. kwa sababu ni nomino zinazo faidi kutokana na vitendo

Mifano zaidi ni:

  1. Anita alimkatia mtoto mkate kwa kisu.( Nani alitendewa ? mtoto)
  2. Shangazi alimnunulia babu yangu koti. (Nani alitendewa? Babu yangu)
Shamirisho
Shamirisho kipozi /yambwa tendwa. ( direct object)
Shamirisho ala/ kitumizi  

Leave a Reply

scroll to top