Konsonanti ni aina ya vitamkwa vitokanavyo na msogeano wa kubana, mwembamba, au wa umadende wa ala za matamshi. Kifonetiki, konsonanti huainishwa kufuatana na kubanwa kabisa kwa mkondohewa katika chemba au kufuatana na kuwepo kwa upenyu mwembamba kiasi cha kuleta msuguano. Katika uchanganuzi wa kifonetiki, sifa bainifu za konsonanti huainishwa kwa kutumia sifa zote hata zile zisizo za lazima, tofauti na uchanganuzi wa kifonolojia ambapo uainishaji wa sifa bainifu huhusisha sifa zile za lazima tu nazo ni: namna ya kutamka, mahali pa kutamkia, hali ya nyuzi sauti, mkao wa kilimi, mkao wa ulimi, na mfumo wa mkondohewa.
A. SIFA YA JINSI YA MATAMSHI
(i) Sifa ya usilabi [+sil]
Irabu za Kiswahili zina sifa ya usilabi, ving’ong’o katika mazingira maalumu vinakuwa na sifa ya usilabi hasa katika mazingira ya kisarufi.
(ii) Mghuno/ughuna [+ghuna]
Nyuzisauti zinapotetemeshwa sauti zitolewazo huwa na mghuno; konsonanti ghuna, vilainisho, irabu, ving’ong’o n.k.
(iii) Ukontinuanti [kont]
Wakati wa kutolewa sauti hizi kuna kuwa na msogeano mpana au mwembamba. Mfano, vikwamizi, irabu, ving’ong’o, viyeyusho na vilainisho n.k.
(iv) Unazali [+naz]
Wakati wa kutolewa kwa sauti hizi hewa huzuiliwa kupita mdomoni na kupitia puani, mfano, [m, n, ŋ,ň]
(v) Utambaza [+tambaz]
Hii huhusika na vitamkwa ambavyo wakati wa kutolewa hewa huzuiliwa na kupita pembeni mwa ala sauti mfano [l]
(vi) Stridenti
Sifa pambanuzi inayohusu sauti zitamkwazo kwa msikiko wa kelelekelele kuliko sauti nyingine. Mfano, [s], [z], [š], [ ], [f], [v], [ts]. Hutamkwa kwa kulazimisha mkondohewa kupita katika sehemu mbili kwa namna ya msuguano ambao hutoa sauti ya kukwamizwa yenye msikiko wa juu.
(vii) Umadende [+mad]
Ni vile vitamkwa vitolewavyo wakati ala sogezi hugongagonga kwenye ala nyingine tulivu, kwa mfano [r].
2. SIFA ZA MAHALI PA MATAMSHI
(a) Ukorona [+kor]
Huhusisha vitamkwa ambavyo wakati wa kutolewa bapa/ ncha ya ulimi huhusika na kuna kuwa na msogeano wa kubana au mwembamba wa ala za matamshi, mfano, sauti za meno, ufizi, kaakaa gumu.
(b) Uanteria [+ant]
Huhusisha vitamkwa vinavyotolewa kwenye ufizi na mbele ya ufizi /t/, /d/, midomo, meno na ufizi.
© Umeno [+meno]
Huhusisha vitamkwa vitolewavyo kwenye meno mfano [th na dh]
(d) Uglota [+glot]
Huhusisha kitamkwa kinachotolewa kwenye glota katikati ya nyuzisauti mfano [h]
3 SIFA BAINIFU ZIHUSUZO KIWILIWILI CHA ULIMI
(i) Ujuu [+juu]
Hii inahusu vitamkwa ambavyo wakati wa kutolewa, ulimi hunyenyuliwa juu ya chemba ya kinywa mfano, [i,u ts ny]
(ii) Uchini [+chini]
Hii huhusisha vitamkwa ambavyo wakati wa kutolewa, ulimi unakuwa chini ya kinywa mfano [a].
(iii) Unyuma [+nyuma]
(iv) Hii hujihusisha na vitamkwa ambavyo hutolewa sehemu ya nyuma ya chemba ya kinywa, mfano, [u, o, k, g, ng].
SIFA BAINIFU NYINGINEZO
UWEKEVU
Katika kubainisha fonimu. Tumia sifa chache kadri iwezekanavyo bayana katika kubainisha fonimu. Mfano,
– ughuna na usighuna
– ukontinuanti/ uendelezi/ vifulizwa
– uanteria
– ukorona
/p/ /b/ /t/ /d/
-gh +gh -gh +gh
-kont -kont -kont -kont
+ant +ant +ant +ant
-kor -kor +kor +kor
(II) UZIADA
Kuwepo au kutokuwepo kwa sifa fulani kunatabirika kutokana na kuwepo au kutokuwepo kwa sifa nyingine. Hususani zile ambazo si muhimu kubainisha fonimu. Kwa mfano,
/i/
+sil
+juu +sil
+son +juu
-chini +son
+mbele
-nyuma
+ghuna
+kont
Sifa za ziada za /i/ ni:
+kont
-chini
-nyuma
+mbele
+ghuna
Sifa za ziada hubainishwa kwa kutumia mantiki. Na huwa si muhimu kubainisha fonimu. Sifa inaweza kubainishwa kwa kutumia uwili unaokinzana. Mfano,
+kont = [-kont]
Mwanamke Mwanamme
[+ke/ -me] [+me, -mke]
Mfano, nazali zote zina ughuna. Pia sauti ambazo ni sonoranti zina sifa ya ughuna. Mantiki inatumika kubainisha sauti zenye sifa ya uziada. Mfano, nazali haiwezi kuwa madende a kiyeyusho.