SIFA PAMBANUZI ZA CHOMSKY NA HALLE

 Sifa zao zilijikita zaidi katika uelekeo wa kifonetiki kuliko walivyofanya Jakobson na Halle. Katika uainishaji wao sifa pambanuzi za sauti za lugha wanazigawa katika makundi matatu.

(i)                 Sauti zenye usonoranti (dhidi ya zile zisizo na usonoranti).

(ii)               Sauti zenye uvokali (dhidi ya zisizo na uvokali).

(iii)             Sauti zenye ukonsonanti (dhidi ya zile zisizo na ukonsonanti)

(i)                 KUNDI LA SONORANTI (dhidi ya zisosonoranti)

Kwa mujibu wa Chomsky na Halle (1968:302) sauti zenye usonoranti hutolewa kwa kuiweka njia ya mkondohewa katika mkao ambao huwezesha ughunishaji wa sauti wa papo hapo, wakati zile zisizo na usonoranti (obstruenti) hutolewa kwa kuiweka njia ya mkondohewa katika mkao ambao hauwezeshi ughunishaji wa papo hapo, mfano, nazali, vitambaza, vimadende na viyeyusho.

(ii)               KUNDI LA V OKALI

Sauti zenye uvokali hutolewa kwa kuweka mkao wa mvungu  wa kinywa katika hali ambayo ubanaji wa mkondohewa hauzidi ule utumikao katika kutamka sauti [i] na [u], na wakati huohuo nyuzisauti zikiwa katika mkao ambao huwezesha ughunishaji wa papohapo.

► Sauti zenye uvokali ni : irabu na vitambaza ghuna, viyeyusho, konsonanti nazali, obstruenti, irabu zisoghuna na vitambaza visoghuna hazina uvokali.

(iii)             KUNDI LA KONSONANTI

Sauti zenye ukonsonanti hutolewa kwa uzuiaji mkali wa mkondohewa katika sehemu ya kati ya njia ya mkondohewa. Sauti zisizo na ukonsonanti hutamkwa bila kuwepo uzuiaji wa mkondohewa wa namna hiyo. Hivyo basi, sauti zenye usonoranti ni: irabu, viyeyusho, nazali, konsonanti na vilainisho. Zenye uvokali: irabu ghuna na vilainisho zenye unazali na konsonanti zisizo na unazali. Baadaye waliona istilahi ya vokali inachanganya wakaanza kutumia istilahi ya USILABI.

hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top