Mfasiri bora anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
1. Awe na ujuzi wa lugha fasaha, hii ina maana kuwa awe anajua kwa ufasaha lugha zote mbili, yaani lugha chanzi na lugha lengwa. Awena umahiri wa lugha mbili zinazohusika; ile uwe mfasiri bora sharti ujue vizuri nyanja mbalimbali za Isimu ya lugha husika kama vile; Fonolojia-Matamshi, Mofolojia-Maumbo, Sintaksia-Muundo na Semantiki-Maana.
2. Awe na ufahamu mkamilifu wa ujumbe au mada iliyoandikwa katika matini chanzi na uwezo au jinsi ya kuelezea ujumbe au mada hiyo kwa ufasaha katika lugha lengwa.
3. Awe amesoma maandishi ya matini chanzi hadi ayafahamu kinaga ubaga halafu aweze kuyafikiria katika lugha lengwa.
4. Awe na maarifa ya TEHAMA (ICT).mfasiri bora lazima awe na maarifa ya teknolojia ile aweze kuimudu vyema kazi yake ya tafsiri.lazima awe na ufahamu wa misamiati ya kisasa ambayo inatumika hasa katika Nyanja ya teknolojia na jinsi baadhi yavyo vinavyofanya kazi
5. Awafahamu watu, jamii na utamaduni wao – mitazamo kuhusu watu, mitazamo – kuhusu wanyama. · Apende kujisomea na kujiendeleza kulingana na mabadiliko ya jamii. Mfano; kusoma vitabu, majarida, magazeti mbalimbali kusikiliza redio na kuangalia TV nk.
6. Awe mwandishi bora.awe ni mtu ambaye anafahamu na kuimuda vyema Nyanja ya uandishi ili aweze kuwasilisha dhana iliyokusudiwa katika matini chanzi,mfasiri lazima awe na ufahamu wa sarufi ya lugha zote mbili anazozishughulikia kwa uketo.
MAREJEO
Cartford [1995] A linguistic Theory Translation
Mwansoko, H.J.M na wenzake [2006] Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na
Mbinu.TUKI.Dar-es-salaam
Newmark, P [1982] Approaches to Translation, Oxford, Pergamon Press
Newmark, P [1988] A Text book of Translation, London, Prentice Hall.
Oxford University Press Dar-es-salaam
Semzaba, E [2006] Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. The General Booksellers LTD.
D.S.M
TUKI [2002] Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TUKI, Dar-es-salaam
TUKI [1985] Kiswahili, Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
www.bakita.org.tz retrieved on Monday 04th July 2018
www.jim-mission.org.uk retrieved on Monday, 04th July 2018
www.ajol.inf retrieved on Monday, 04th July 2018
Vitabu vilivyotafsiriwa ambavyo vimetumika kama marejeo
Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa, kimetafsiriwa na Abdilatif Abdalla
Ferdinand Oyono: House boy, Kimetafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele.
William Shakespeare: Juliasi Kaizari: Kimetafsiria na Julius K. Nyerere
Mabepari wa Venisi: Kimetafsiriwa na Julius K. Nyerere
Hekaya za Abunuwasi: Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa
Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton
Sir Rider Haggard: Mashimo ya Mfalme Suleiman