Silabi ni tamko moja katika neno/herufi moja au zaidi ambazo hutamkwa pamoja.
Silabi pia inaweza fasiriwa kuwa ni kipashio cha lugha kinachotamkika, au silabi ni mapigo ya sauti katika neno. kwa mfano neno Kalamu lina silabi tatu, nazo ni Ka-la-mu.
jedwali hili linaonyesha mifano zaidi ya silabi katika maneno mbalimbali:
Neno | Silabi | Idadi ya silabi |
Aliondoka | a-li-o-ndo-ka | 5 |
Kalamu | ka-la-mu | 3 |
hufikirii | hu-fi-ki-ri-i | 5 |
anasoma | a-na-so-ma | 4 |
Aina za silabi
Silabi wazi/huru
Hizi ni silabi zinazoishia kwa vokali. Nyingi kati ya silabi hizi ni zenye asili ya Kibantu.
Mathalan:
ba/ba = baba
sha/nga/zi = shangazi
Silabi funge
Hizi ni silabi zinazoishia kwa konsonanti. Aghalabu asili ya silabi hizi ni lugha za kigeni.
Ghalibu, silabi hizi hujitokeza sehemu ya kati ya neno.
Mathalan :
/lab/ da = labda
/il/ hali = ilhali
/daf/ tari = daftari
/dik/ teta = dikteta.
Miundo ya Silabi za Kiswahili
i. silabi ya irabu pekee
oa o-a
ua u-a
ii. silabi za konsonanti na irabu
Soma so-ma
iii. silabi za konsonanti mbili na irabu / Silabi ambatano
Silabi hizi hujumuisha consonanti mbili kisha irabu Kwa mfano mwa-mba , mwa-li-mu
o-ndo-ka
iv. silabi za konsonanti tatu na irabu / Silabi changamano
Hujumuisha konsonanti tatu na irabu moja kwa mfano mbwe- ha
v. silabi za konsonanti pekee
Mchicha m-chi-cha
Kelbu
Kuran
vi. Silabi za irabu na konsonanti
ah!,
vii. Silabi za konsonanti, irabu na konsonanti
Zoezi
- Ukitoa mifano, fafanua miundo miwili ya silabi za Kiswahili.
- Tenganisha silabi katika maneno yafuatayo:
- inkisari
- baiskeli.