Tafsiri inauhusiano mkubwa na taaluma nyingine au vipengele vingine kama ifuatavyo: Ina uhusiano na isimu linganishi; (comparative linguistics)
v Isimu linganishi hijishughulisha na kulinganisha vipengele mbalimbali vya kiisimu vya lugha mbili au zaidi, pamoja na kuchunguza mbinu za ulinganishi huu. Uhusianao wake na tafsiri;- humsaidia mfasiri kuelewa mifumo ya lugha mbalimbali na jinsi luhga hizo zinavyotumia vipengele vyake vya kiisimu kutolea taarifa mbalimbali.
v Isimu jamii.
isimujamii;- Isimujamii inahusika na kuchunguza uhusiano kati ya lugha fulani na jamii ambayo inatumia lugha hiyo. Rejesta mbalimbali za kijamii pamoja na maingiliano baina ya lugha. Ujuzi wa isimujamii unamsaidia mfasiri kufahamu athari zinazotokana na mahusiano baina ya lugha na jamii husika na kuzingatia mambo mbalimbali katika kutafsiri.
v semantiki/pragmatiki
semantiki/pragmatiki;- Semantiki ni taaluma inayochunguza maana ya maneno katika upweke na katika makundi/taaluma inayochunguza maana ya maana. Kwa kuwa kinachotafsiriwa ni mawazo au maana ya matini (siyo neno pwekepweke) basi ujuzi huu wa semantiki utamwezesha mfasiri kujua au kung’amua kuwa maana ya matini hiyo haitokani na maana ya neno mojamoja badala yake inatokana na maana ya kimatumizi kwa ujumla katika mktadha mahususi.
v elimumitindo
elimumitindo (stylistics);- Hii inahusu uainishaji wa mitindo mbalimbali ya lugha na miktadha ya matumizi yake. Elimumitindo Mitindo Mazingira ya kutumia Uhusiano wake na tafsiri;- Taaluma hii ya elimumitindo itamwezesha mfasiri kubaini mtindo wa matini chanzi ambao haunabudi kuhamishiwa katika matini lengwa. Inauhusiano na mantiki (logic);- Mantiki inahusu ukweli na uhakika au usahihi wa mambo kama inavyosemwa, kuandikwa au kuaminika kwa watu. Mantiki humsaidia mfasiri kubaini kauli zisizo dhahiri na zinazokanganya katika matini chanzi ili azirekebishe kwanza kabla ya kuanza kutafsiri. Kwa mfano; Kenya got the new consitutoon in the year 1993.
MAREJEO
Cartford [1995] A linguistic Theory Translation
Mwansoko, H.J.M na wenzake [2006] Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na
Mbinu.TUKI.Dar-es-salaam
Newmark, P [1982] Approaches to Translation, Oxford, Pergamon Press
Newmark, P [1988] A Text book of Translation, London, Prentice Hall.
Oxford University Press Dar-es-salaam
Semzaba, E [2006] Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. The General Booksellers LTD.
D.S.M
TUKI [2002] Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TUKI, Dar-es-salaam
TUKI [1985] Kiswahili, Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
www.bakita.org.tz retrieved on Monday 04th July 2018
www.jim-mission.org.uk retrieved on Monday, 04th July 2018
www.ajol.inf retrieved on Monday, 04th July 2018
Vitabu vilivyotafsiriwa ambavyo vimetumika kama marejeo
Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa, kimetafsiriwa na Abdilatif Abdalla
Ferdinand Oyono: House boy, Kimetafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele.
William Shakespeare: Juliasi Kaizari: Kimetafsiria na Julius K. Nyerere
Mabepari wa Venisi: Kimetafsiriwa na Julius K. Nyerere
Hekaya za Abunuwasi: Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa
Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton
Sir Rider Haggard: Mashimo ya Mfalme Suleiman