TAFSIRI NA UKALIMANI

 Tafsiri [Translation]

Translation is the process of transferring meaning of written text from one language into another. While the translator is an individual or computer program that renders a text into another language. 

Dhana ya Tafsiri.[the concept of translation]

Tafsiri ni nini?

Tafsiri imefasiliwa kuwa, ni Kutoa mawazo kutoka katika lugha moja kwenda lugha nyingine bila ya kubadilisha maana. [TUKI 2002: 271]

Catford [1965:20] anasema tafsiri ni, “Kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja {lugha chanzi} na kuweka badala yake mawazo yanayolingana katika lugha nyingine {lugha lengwa}.

Vilevile imefasiliwa kuwa ni “Mawazo yaliyotolewa kutoka lugha moja hadi lugha nyingine.”

TUKI [2002: 271] Tafsiri ni kueleza maana ya maneno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine.

Newmark (1982) Tafsiri ni jaribio la kuwasilisha ujumbe ule ule ulioandikwa katika lugha moja kwa lugha nyingine. Jaribio kwa sababu si mara zote unaweza kufanya hivyo kwani unaweza kushindwa au kufaulu. * Udhaifu wa Newmark katika fasili yake ni kwamba hakuzingatia umbo la kazi yenyewe au mtindo wa kazi yenyewe. Mfano; kadi ya mwaliko, barua nk. Mwansoko na wenzake (2006) Tafsiri ni zoezi la uhawilishaji (Transferring) wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi lugha nyingine. * Ukiangalia wataalamu hawa wawili utaona kwamba wanafanana; kwani wanaona kuwa tafsiri hufanywa katika maandishi. Nida na Taber (1969) wanaona kuwa tafsiri hujumuisha upya ujembe wa lugha chanzi kwa kutumia visawe asilia vya lugha lengwa vinavyokaribiana zaidi na lugha chanzi, kwanza kimaana na pili kimtindo. Kwa mfano; “Damu nzito kuliko maji” – “Blood is thinker than water”. Ndugu yako ni muhimu zaidi kuliko mtu mwingine. “Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni” – “Wonders never end” * Nida na Tiber wanaona kuwa katika tafsiri kitu muhimu ni kuzingatia maana na mtindo.

Maana zote hizo tulizoziangalia, utaona kuwa, kuna mambo matatu muhimu yanayojitokeza, mambo hayo ni:

(i) Mawazo yanayotakiwa kutafsiriwa sharti yawe katika maandishi.

(ii) Mawazo au ujumbe kati ya lugha chanzi na lugha lengwa sharti yalingane.

(iii) Tafsiri inaweza kuwa kutoa maana ya maneno au mawazo.

Baada ya kuangalia maana ya tafsiri, sasa tuangalie maana ya mfasiri na sifa anazotakiwa kuwa nazo mfasiri:

Mfasiri

Mfasiri ni mtu anayefanya tafsiri kutoka lugha moja hadi lugha nyinge.[TUKI:2000:165]

Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa ni mtu yeyote anayejishughulisha na kazi za kutafsiri. Ni mtu mwenye taaluma au ujuzi wa kutafsiri na ambaye anajishughulisha na kazi hizo



MAREJEO

Cartford [1995] A linguistic Theory Translation

Mwansoko, H.J.M na wenzake [2006] Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na

Mbinu.TUKI.Dar-es-salaam

Newmark, P [1982] Approaches to Translation, Oxford, Pergamon Press

Newmark, P [1988] A Text book of Translation, London, Prentice Hall.

Oxford University Press Dar-es-salaam

Semzaba, E [2006] Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. The General Booksellers LTD.

D.S.M

TUKI [2002] Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TUKI, Dar-es-salaam

TUKI [1985] Kiswahili, Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

www.bakita.org.tz retrieved on Monday 04th July 2018

www.jim-mission.org.uk retrieved on Monday, 04th July 2018

www.ajol.inf retrieved on Monday, 04th July 2018

Vitabu vilivyotafsiriwa ambavyo vimetumika kama marejeo

Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa, kimetafsiriwa na Abdilatif Abdalla

Ferdinand Oyono: House boy, Kimetafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele.

William Shakespeare: Juliasi Kaizari: Kimetafsiria na Julius K. Nyerere

Mabepari wa Venisi: Kimetafsiriwa na Julius K. Nyerere

Hekaya za Abunuwasi: Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa

Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton

Sir Rider Haggard: Mashimo ya Mfalme Suleiman


hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top