Tofauti kati ya fasihi na sanaa nyingine

  1. Fasihi hutumia lugha kama malighafi ya kuelezea fikira za binadamu. Sanaa nyingine
    hazitumii lugha. Tanzu na vipera vya fasihi hutumia lugha ya kitamathali kama vile nahau, misemo, misimu, lakabu, kinaya na dhihaka kulelezea hali au jambo.
  2. Fasihi, tofauti na sanaa nyingine, hujikita katika mazingira au muktadha wa mahali, wakati na hali maalumu.
  3. Fasihi ni sanaa tendi. mwasilishaji wa fasihi simulizi anaweza kuigiza yale anayowasilisha na pia akashirikisha hadhira yake kwa kuigiza. Sanaa nyingine, kama vile ufinyanzi na uchongaji,haziigizwi.
  4. Fasihi hutumia wahusika kuwasilisha maudhui. Ngano, riwaya, tamthilia, baadhi ya mashairi na hadithi fupi ni mifano ya kazi zinazotumia wahusika kuwasilisha maudhui. Sanaa nyingine, kama vile uchongaji, ni maumbo yanayomithilisha watu, hali na vitu mbalimbali katika jamii.
  5. Fasihi huwasilisha ujumbe kwa kutumia maudhui na fani pamoja, tofauti na sanaa nyingine ambazo hutumia sura au maumbo ya vitu.

Leave a Reply

scroll to top