Tofauti ya Kiambishi na Mofimu

Ikumbukwe kuwa kiambishi ni mofimu ambayo huongezwa kabla au baada ya mzizi wa neno ili kuwakilisha dhana fulani.Pia,kiambishi hujitokeza kama mofimu tegemezi. Tofauti kuu hapa ni kuwa mofimu huweza kujisimamia kiimaana(mofimu huru) ilhali kiambishi hutegemea viambishi vingine ili kukamilisha maana.

Viambishi

Viungo vyenye maana vinavyofungamanishwa na mzizi wa neno ili kulipa maana mbalimbali.Mofimu hizo hupachikwa nyuma au mbele ya mzizi wa neno ili kubadilisha dhana ya neno. Kwa kuwa mofimu hizo hupachikwa sehemu tatu tofauti, tunapata aina mbili za viambishi kwa mujibu wa nafasi zake katika neno, yaani; viambishi awali ambavyo hupachikwa mwanzoni au nyuma ya mzizi wa neno,  na viambishi tamati ambavyo hivi hupachikwa mbele au mwishoni mwa mzizi wa neno.

Leave a Reply

scroll to top