Uakifishaji ni neno linalotumiwa kuelezea matumizi ya alama mbalimbali katika maandishi ili kuboresha na kufanikisha mawasiliano. Zipo alama mbalimbali zinazitumiwa ili kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe nazo ni:
- Alama za usemi(“”)
- Dukuduku (…)
- Koma/mkato/kipumuo( , )
- Ritifaa/kibainishi( ’ )
- Mshazari/mkwaju(/)
- Kistari kifupi( – )
- Kistari kirefu
- Mstari( ___ )
- Kikomo/kitone/nukta (.)
- Nusu/semi koloni/nukta na kituo (;)
- Vifungo/mabano/paradesi( )
- Herufi kubwa(H)
- Herufi ndogo (h)
- Koloni/ Nukta mbili ( : )
- Hisi/mshangao (!)
- Herufi nzito (h)
- Herufi za mlazo/italiki(h)
- Kinyota(*)
- Swali/Kiulizo