UCHAMBUZI WA MASHAIRI

 

Katika uchambuzi wa mashairi,
vipemgele vifuatavyp huzingatiwa;

  • Dhamira
  • Maudhui
  • Muundo
  • Lugha

a) Dhamira

Dhamira ni lengo kuu ambalo mtunzi
wa shairi huwa nalo anapoitunga kazi yake. Lengo hilo linaweza kuwa kuelimisha
jamii, kuikosoa jamii, kutahadharisha, kufariji, kuhamasisha n.k

 Maneno mengine ambayo huweza
kutumika badala ya dhamira ni kama vile lengo,
nia, kusudi au azma
.

Mara nyingi, wanafunzi hukumbana na
swali hili…‘Eleza dhamira ya shairi hili.’

b) Maudhui

 Maudhui ni ujumbe mkuu
unaowasilishwa katika  kazi ya fasihi. Maudhui huweza kuwa kama vile ya
ndoa, migogoro, elimu, matabaka, ukengeushi n.k

c) Muundo

Muundo ni umbo au sura ya shairi.
Umbo hubainishwa kwa kuonekana bayana kama alivyoandika mtunzi. kwa
kawaida  mwanafunzi huulizwa…‘Eleza muundo wa hili shairi.’anapolijibu
swali hili anastahili kuangalia shairi na kuandika tu anayoyaona. Hastahili
kufikiria kwa kina ilikuandika anayoyaona. 

Mambo yafuatayo huzingatiwa
mwanafunzi anapoeleza muundo wa shairi;

         Je
shairi lina beti ngapi?

         Je
shairi lina mishororo mingapi katika kila ubeti?

         Je
shairi lina vipande vingapi katika kila mshororo?

         Je
shairi lina vina vya kati na vya nje, na kuna urari wa vina au

la?

         Je
idadi ya mizani ni ngapi katika kila kipande au mshororo?

         Shairi
lina kibwagizo au kituo? Iwapo lina kibwagizo, basi nakili

kibwagizo moja kwa moja

d) Lugha

Jinsi mtunzi wa mashairi mmoja
anavyotumia lugha ni tofauti

na na jinsi mtunzi mwingine
atakavyoitumia. Kipengele hiki cha lugha  huchunguza

jinsi mtunzi ametumia tamathali za
usemi. 

Lugha pia huendeleza maudhui ya
shairi. Tamathali hizi ni pamoja na;

v       Tashbihi/mshabaha– ni mbinu ya
lugha ambapo vitu viwili

hulinganishwa kwa njia isiyo ya moja
kwa moja. Kwa ufupi,ni ulinganisho

isiyo wa moja kwa moja kwa kutumia
vilinganishi kwa mfano: mithili

ya, kama, ja na sawa na. 
Tazama mfano huu:

Maria ni mfupi mithili ya/ja nyundo.

v       Uhaishaji/uhuishi/tashihisi– ni
mbinu ambayo vitu visivyo na uhai

hupewa sifa za kibinadamu. Mfano:
giza likammeza mzima mzima.

v       Misemo na nahau- ni kauli
fupifupi ambazo hutumika kutoa maana

nyingine pasi na maana
iliyotumika. 

         
            Misemo huwa
haitumii vitenzi kwa mfano: mkono birika- mchoyo, mkono mrefu-mwizi n.k. 

         
              Nahau hutambulishwa
kwa matumizi ya vitenzi kwa mfano: kula kalenda-fungwa jela, chungulia kaburi-
karibia kifo n.k

v       Takriri/anafora– mbinu ya
kurudiarudia neno,tukio au mawazo Fulani.Takriri huweza kuwa za aina mbalimbali
kama vile 

Takriri sauti- sauti fulani
hurudiwarudiwa.

Takriri   neno-
neno/kifungu cha maneno fulani hurudiwarudiwa,

Takriri mawazo- mawazo fulani
hurudiwarudiwa.

Takriri muundo/usambamba ambapo
muundo fulani wa

kisintaksia hurudiwarudiwa. Malenga
hutumia takriri hususan

kusisitiza ujumbe.

v       Maswali balagha/mubalagha– huwa ni
maswali yasiyohitaji majibu.

v       Tanakuzi– pia huitwa ukinzani. Hapa mawazo yanayokinzana hutumiwa
pamoja katika sentensi moja. Kwa mfano; baada ya dhiki faraja, mpanda 
ngazi hushuka, nazama nakuibuka.

v       Tanakali za sauti– mbinu hii pia
hujulikana kama onomatopeia. Maneno yanayoiga sauti au hali fulani hutumika.
Mfano kuanguka majini chubwi. 

v       Methali– huwa ni misemo ya hekima
na ambayo maana yake imefumbwa. 

v       Chuku/udamizi– ni mbinu ya kutilia
chumvi suala fulani kwa ajili ya kusisitiza ujumbe fulani.

v       Tasfida– ni matumizi ya lugha ya
adabu ili kuficha makali ya lugha. Mfano kujifungua mtoto badala ya kuzaa,
kuenda haja badala ya kuenda chooni.

v       Kinaya– hapa mtunzi huleta dhana
ya kinyume cha matarajio. Kwa mfano badala ya kiongozi alichaguliwa kutetea
maslahi ya watu wake akawa wa kwanza kuwanyanyasa. Kuna aina kadhaa za kinaya
kama vile kinaya cha kiusemi na kinaya hali. Kinaya cha kiusemi ni hali ambapo
maana inayokusudiwa huwa kinyume cha kile kinachosemwa. Katika kinaya hali
matokeo huwa kinyume cha matarajio.

v       Jazanda– matumizi ya lugha fiche
au ya mafumbo. Msomaji huhitajika  kuwaza maana kamili iliyokusudiwa. Kwa
mfano paka na panya kwa maana ya watawala na watawaliwa.

v       Tabaini– matumizi ya neno “si”
pamoja na maneno kinzani. Kwa mfano: Alikuwa si wa maji si wa dawa.

v       Utohozi- mbinu ya
kuswahilisha maneno yasiyo ya lugha ya Kiswahili.Mfano “school”- skuli,
“Class”- klasi

v       Sitiara/sitiari– huu ni
ulinganisho wa vitu au hali mbili kwa njia ya moja kwa moja kwa sababu vitu
hivi vina sifa au tabia sawa. Mfano: Mwalimu mkuu ni simba, Maria ni twiga.

v       Taashira/Ishara – mbinu
ambapo mtunzi hutumia lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Kwa mfano mvi
kuashiria mtu mzee.

v       Taswira– ni mbinu ambapo mtunzi
hutoa maelezo ambayo huibua picha ya kitu au hali fulani akilini mwa msomaji.
Kuna aina kadha za  taswira kama vile: 

Taswira mnuso/harufu- k.m rihi ya
maua

Taswira mguso- k.m kumpapasa, kumbusu
miguu

Taswira usikivu- k.m anasikiliza
ndege

Taswira ya mwendo- k.m yeye
kuendelea kwa furaha  

v       Nidaa/siahi– hutambulishwa na
matumizi ya alama hisi (!) ambayo 

mtunzi hutumia kudhihirisha hisia
fulani kama vile furaha, huzuni,

mshangao n.k

v       Majazi– mbinu ya mwandishi kuwapa
wahusika ama mahali majina

yanayoshabihiana na tabia, vitendo
au hali zao. 

Vigezo vingine muhimu katika uchambuzi wa mashairi

Kichwa cha shairi

Uteuzi wa anwani huzingatia urudiaji
wa maneno fulani katika shairi lote au pia kibwagizo. Hivyo basi mwanafunzi
anaweza kulipa shairi anwani kwa kuzingatia ni maneno yapi yaliyorudiwarudiwa
au kwa kutumia maneno katika kibwagizo. Anwani ya shairi pia yaweza kubuniwa
kutokana na maudhui yanayojitokeza kwa wingi katika shairi. Anwani ya shairi
huwa kama ufupisho au muhtasari wa yale yaliyomo katika shairi. Hivyo basi mtu
yeyote anayesoma kichwa cha shairi fulani huweza kukisia kile ambacho shairi
hilo linazungumzia hata bila ya kulisoma shairi lenyewe. Kwa ufupi, kichwa cha
shairi humpa msomaji taswira ya kijumla ya mambo yanayozungumziwa katika utungo
wenyewe.

Falsafa ya mwandishi

Huu ni msimamo wa mwandishi kuhusu
maudhui tofauti tofauti aliyoyajadili katika utungo wake. Msimamo wa mwandishi
unaweza kuwa analiunga mkono jambo fulani au analipinga jambo fulani. Hili
litadhihirika wazi jinsi anavyoeleza maudhui yake.

Nafsineni

Huwa ni anayezungumza katika shairi.
Wakati mwingine huwa ni mtunzi mwenyewe anayezungumza au wakati mwingine
akamtumia mhusika fulani kupasha ujumbe wake.

Nafsi nenewa/hadhira lengwa

Huwa ni anayeelekezewa ujumbe.
Ujumbe katika shairi au hata kazi yoyote ya fasihi huwa inamlenga mtu au kundi
fulani la watu. Walengwa hawa ndio nafsi nenewa ama hadhira lengwa, kwa mfano
wanafunzi, wazazi au wananchi.

Lahani/Toni ya shairi

 Toni ni hisia ambazo huibuka
kutokana na yale anayosema mzungumzaji katika shairi. Mzungumzaji huweza kuibua
hisia za kuchekesha, kulalamika, kubeza, furaha, huzuni n.k

Mandhari na wakati

Mandhari ni mazingira au muktadha au
mahali ambapo shairi fulani hutungiwa.Mandhari na wakati huenda sambamba.
Kutokana na maudhui ya shairi,tunaweza kubaini ni wapi na ni lini shairi
lilitungwa. Mifano ya mandhari ni kama vile Pwani, mjini, shuleni n.k. Hivyo
basi mandhari na wakati husaidia kuendeleza maudhui ya shairi. Kwa mfano katika
shairi la Mnazi na Vuta n’uvute, mandhari ni ya Pwani.

Uhusika katika ushairi

Mashairi pia huweza kuwa na wahusika
haswa tukirejelea ngonjera na malumbano hivyo basi ni muhimu kulitilia maanani
suala hili. Wahusika huwa kama sauti ya mwandishi maanake ni kupitia kwao
ambapo mtunzi hueleza mawazo yake bayana.

Tasnifu

Haya ni maelezo mafupi ambayo
mwandishi wa kazi ya fasihi huyatoa kuhusu maudhui na dhamira yake katika
utungo.

Lugha ya nathari/Lugha
tutumbi/mjalizo

 Lugha ya nathari ni lugha ya
kawaida. Huwa ni maandishi mfululizo. Ubeti uandikwe kwa aya moja ama kwa njia
ya kiinsha bali si ya kishairi. Mishororo igeuzwe iwe sentensi za iswahili
sanifu zinazozingatia kanuni za lugha. Sehemu zilizorudiwarudiwa ziandikwe mara
moja tu. Usitumie lugha ya mshairi.

 

     

USHAIRI

1.        

Historia ya Ushairi

2.        

Changamoto za ufundishaji na usomaji wa uhairi

3.        

Istilahi zinazotumika katika ushairi

4.        

Sifa za mashairi ya kimapokeo

5.        

Sifa za mashairi huru

6.        

Kategoria kuu za mashairi

7.        

Bahari za mashairi

8.        

Uchambuzi wa mashairi

9.        

Uhuru wakishairi

 

hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top