UHURU WA KISHAIRI

Uhuru wa mshairi

Uhuru wa kishairi ni idhini yamwandishi kutunga shairi kwa namna fulani bila kuzingatia kanuni za kisarufi.Uhuru wa kishairi huhusisha yafuatayo:

1) Mazida 

Uhuru huu humruhusu mtunzi kuyarefusha maneno fulani.Mazida husaidia kuleta utoshelezo wa idadi ya mizani katika kipande au mshororo na pia urari wa vina.

2) Inkisari 

 Huu ni uhuru wa mshairi kuyafupisha maneno fulani.Inkisari pia husaidia kutosheleza idadi ya mizani

na kuleta urari wa vina.

3) Tabdila 

Ni uhuru wa mshairi kubadilisha herufi au hata sauti ya neno bila kubadili maana ya neno hilo. Kwa mfano daraza badala ya darasa.Tabdila husaidia kuleta urari wa vina katika kipande cha mshororo.

4) Kuboronga/kufinyanga/Kubananga sarufi 

 Pia huitwa miundongeu/ukiushi wa kisintaksia/ukiushi wa kimiundo. Huu ni uhuru wa mshairi kutofuata kanuni zinazotawala sarufi. Kusudi la kufanya hivi ni kuleta urari wa vina katika mishororo. Kwa mfano, kunapopambazuka kila, amka mwanadamu badala ya kila kunapopambazuka, mwanadamu amka

5) Kikale 

Ni matumizi ya msamiati wa kale, kwa mfano, Ngeu badala ya damu, nyuni badala ya ndege, mgunda badala ya shamba n.k

6) Vilugha/vilahaja 

Ni matumizi ya msamiati wa lahaja za Kiswahili badala ya Kiswahili sanifu.

7) Utohozi

 Kutohoa ni kuswahilisha msamiati wa lugha nyingine na kuwa Kiswahili. Kwa mfano, klasi badala ya class, eropleni badala ya aeroplane, deski badala ya desk n.k.

          

       USHAIRI

1.      
 

Historia ya Ushairi

2.      
 

Changamoto za ufundishaji na usomaji wa uhairi

3.      
 

Istilahi zinazotumika katika ushairi

4.      
 

Sifa za mashairi ya kimapokeo

5.      
 

Sifa za mashairi huru

6.      
 

Kategoria kuu za mashairi

7.      
 

Bahari za mashairi

8.      
 

Uchambuzi wa mashairi

9.      
 

Uhuru wakishairi

1

 





 


hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top