MOFOLOJIA
► Ni taaluma inayochunguza maumbo ya maneno katika lugha yaani namna neno linavyoundwa.
Kipashio chake cha msingi ni MOFIMU ambacho hakiwezi kugawanyika mara mbili na kuleta maana ya kileksika ama kisintaksia, kwa mfano
Mama
●Mofimu leksika/huru
m/toto
●m- ni kiambishi cha idadi
●toto mofimu ya mzizi
UHUSIANO
►Taaluma zinahusika na lugha mahsusi/maalumu
► Mofimu ambazo ni vipashio vya msingi huundwa na fonimu.
► Mofimu moja inaweza kuwa na maumbo mbalimbali→ALOMOFU
Kwa mfano
Mtoto, muuguzi, mwalimu
Kuna m, mu, mw ambazo ni mofimu za umoja nazo ni alomofu za mofimu ngeli ya kwanza umoja. (YUAWA).
►Fonimu ni kipande tu cha sauti yaani umbo la kitamkwa kimoja wakati mofimu yaweza kuwa umbo la silabi, mofimu au neno.