Sintaksia ni taaluma ihusikayo na mpangilio wa maneno katika tungo. Kipashio cha msingi katika sintaksia ni neno. Kipashio cha juu katika sintaksia ni SENTENSI. Aidha sentensi huundwa kwa maneno yaliyoundwa na mofimu. Maneno hayo pia huunda kirai+kishazi+sentensi.
Kuna kanuni za kifonolojia zinazotawala miundo ya tungo hizo.
Neno lazima likubaliane na mpangilio wa silabi na fonimu
Kuna kanuni fulani zitumikazo ili kupata muundo fulani wa maneno, kwa mfano
Mke wake mkewe. Uunganishaji na udondoshaji ni kanuni za kifonolojia.