Nomino za Kiswahili zinaweza kuwa katika hali ya wastani (kawaida), Ukubwa na hata udogo.Nomino zikiwa katika hali ya udogo huwa na maana kuwa kitu kinachotajwa kimedharauliwa au kimedunishwa. vile vile, nomino zikiwa katika hali ya ukubwa huleta dhana
kuwa kitu kinachotajwa kimekuzwa na kinachukiza.Tanbihi : ni vyema kufahamu kuwa nomino zikibadilika kutoka hali ya wastani hadi ile ya udogo na ukubwa huingia katika ngeli ya LI-YA, ukubwa, na KI-VI, udogo.
pia Katika hali ya ukubwa na hata udogo, sauti za nazali za nazali /n/, /m/, /ny/ na /ng’/ hudondolewa na huku kiambishi ji kikichukua nafasi ya nazali zinazohusika katika ukubwa na kiji/ki katika udogo
Mifano:
Wastani | Ukubwa | Udogo |
Mkono | jikono | kikono |
Mguu | kiguu | Guu/Jiguu |
Njia | jia | kijia |
nguo | Guo | kiguo |
Uso | juso | Kijuso |
1.Wastani: Ng’ombe yule amechinjwa.
Udogo: Kigombe kili kimechinjwa .
Ukubwa: g’ombelile limechinjwa
2. Wastani: Mkono wake umevunjika
Udogo: Kikono chake kimevunjika
Ukubwa: Jikono lake limevunjika