Umuhimu wa lugha

  •   Ni kitambulisho cha jamii: Huwatambulisha watu watokao katika janibu fulani hasa Afrika Mashariki.
  • Ni nyenzo ya Kufundishia- Lugha hutumika katika kufundishia elimu.
  • Lugha hufanikisha mawasiliano: Hutumiwa kupitisha ujumbe kutoka mtu mmoja hadi mwengine. 
  •  Lugha huleta uwiano: Huunganisha wananchi kwa kuwaleta pamoja kama lugha ya taifa. 
  • Ni nguzo kubwa katika kuimarisha biashara hivyo kuendeleza biashara baina ya watu maanake kuna uelewano. 
  • Lugha huendeleza utamaduni katika jamii kwa kupitisha lugha kutoka kizazi kimoja hadi kingine, lugha hukuza na kuendeleza utamaduni wa jamii husika.
  • Lugha huendeleza kazi ya sanaa, hasa inapohusu kuwaelezea waja ujumbe muhimu.Lugha hutumika kuelezea hisia za binadamu. 
  • Huweza kusuluhisha migogoro mbalimbali itokeapo kati ya waja kutoka tabaka tofauti tofauti hivyo kuleta muafaka.
  • Kuunganisha- Lugha hupatanisha na kuleta uelewano miongoni mwa wanajamii. Pia lugha huweza kutofautisha jamii moja na nyengine.

Leave a Reply

scroll to top