Upambanuzi wa sentensi sahili

Upambanuzi wa sentensi sahili huhusisha kuonyesha wazi namna ilivyoundwa. Kielelezo mstari ni mbinu ya kuipambanua sentensi na hutokea kwenye mstari mmoja. Kutokea kwa upambanuzi huu katika mstari moja ndiko kunaufanya kuitwa upambanuzi wa kielelezo mstari.

Hatua za upambanuzi wa sentensi kwa kutumia kielelezo mstari ni;

i. Tambua kikundi nomino (KN) na kikundi tenzi (KT).

ii. Bainisha aina za maneno zilizotumiwa katika KN na KT.

tanbihi: Kama sentensi ina kikundi tenzi pekee, unastahili kutumia kapa (θ) kuonyesha kuwa kundi nomino halipo. Yaani KN (θ). Kapa hutumiwa kuonyesha kuwa kipashio kilichotajwa hakipo.

Baadhi ya alama zitumiwazo katika upambanuzi wa sentensi sahili ni:

(θ) alama kapa ikimaanisha Kilichoonyeshwa hakipo (hakionekani).

—> Mshale ambao humaanisha,hubadilika na kuwa

S – sauti /S/ ambayo husimamia sentensi, sentensi ni neno au fungu la maneno lenye kiima na kiarifu na huwa na maana kamili.

Mifano katika sentensi:

  1. mwanafunzi anasoma kitabu kizuri . S—>KN(N)+KT(T+N+V)
  2. Maria na Koome wanapenda kusoma sana. S —>KN(N+U+N)+KT(Ts+T+E)
  3. Magaidi wamevamia nchi yetu. S—> KN(N)+KT(T+N+V)
  4. Cherono, Omari na Andayi wameandika ikitabu kizuri. S—> KN(N+N+U+N)HKT(T+N+V)
  5. Kiatu kizuri kimeraruliwa sana. S—>KN(N +V}KT(T+E)

Leave a Reply

scroll to top