Usemi Halisi na Usemi wa taarifa

Usemi Halisi

Usemi halisi hutumiwa kuelezea maneno halisi kama yanavyotamkwa na msemaji.Hutumiwa kuelezea kauli,maneno, au matamko yanayosemwa na mtu mwenyewe. Huwa ni maneno yanayosemwa na mtu moja kwa moja na huwa katika wakati uliopo. Katika usemi huu yafuatayo huzingatiwa;
– Usemi halisi huandikwa bila kugeuza chochote.
– Huanzia kwa herufi kubwa.
– Hunukuliwa kwa alama za usemi ambazo huandikwa zikiwa mbili mbili na moja moja katika dondoo ndogo k.m. “Mwambie ‘ugua pole’ ukimuona,” baba aliniambia.
– Koma hutumiwa mwanzoni au mwishoni mwake.
– Msemaji mpya anapoanza kusema, unapaswa kufungua aya mpya k.m.
Alimuuliza, “Huendi kwa nini?”
“Sikupewa ruhusa,” alijibu Zahara.
– Alama ya hisi,kiulizo,koma,nukta za dukuduku na kituo kikuu pia hutumiwa pamoja na alama za mtajo na ni lazima zije kabla ya alama za kufunga. m.f
“Unanidanganya?”

-Kauli moja ikivunjwa katika vitengo, kitengo cha pili hata baada ya kuwekewa alama za kufungua ,neno lake la kwanza litaanza kwa herufi ndogo isipokuwa neno lilo likiwa nomino maalum
Usemi wa Taarifa
Usemi wa taarifa ni ripoti kuhusu mambo yaliyosemwa na mtu mwingine.
Si lazima maneno yatokee yalivyosemwa. Yanaweza kubadilishwa mradi ujumbe ubakie ule ule.
Alama za mtajo, kiulizi na hisi hazitumiki.
Maneno “kwamba’ na ‘kuwa’ hutumiwa.
Baadhi ya maneno na viambishi hubadilika. K.m

Usemi Halisi – ” Ninaishi karibu na hospitali,” Maria alisema.

Usemi wa taarifa – Maria alisema kuwa anaishi karibu na hospitali.

Usemi Halisi – Mama alisema, ” Watoto wangu nitawaombia dua kwa mwenyezi mungu.”

Usemi wa taarifa – Mama alisema kuwa angewaombea watoto wake kwa mwenyezi mungu.

Leave a Reply

scroll to top