Viambishi Tamati
Ni viambishi mbavyo hutokea baada ya mzizi k.m. ki-pig-ishw-a-cho
navyo ni kama vifuatavyo:
Viambishi tamati huwa na majukumu mbali mbali kama ifuatavyo;
i. Viishio
Katika kauli ya kutenda, vitenzi vyenye asili ya Kibantu huishia kwa sauti -/a/. Kwa mfano: a-na-omb-a, tu-li-zo-andik-a
Tanbihi: Tunapokanusha vitenzi hivi vyenye asili ya Kibantu katika wakati uliopo na wakati wa mazoea kiishio /-a/ hubadilika na kuwa /i/ Kwa mfano: ‘ Ha-pat-ik-an-i, Si-ku-ju-i ”
Vitenzi vyenye asili ya kigeni huchukua viishio tofauti kama vile ‘e’, ‘i’na ‘u’ katika kauli ya kutenda. Kwa mfano: ha-wa-ja-tu-jib-u, a-na-tu-subir-i, ni-me-ku-sameh-e Hata hivyo katika kauli nyinginezo (isipokuwa kauli ya kutenda) vitenzi hivi vya kigeni huchukua kiishio “a”. k.m harib-ik-a, tu-me-jib-iw-a
ii. Mnyambuliko wa Vitenzi
Kunyambua kitenzi ni kukiongeza viambishi tamati ili kukipa maana tofauti.
kwa mfano Vunj-ik-a kauli ya kutenda, vinj-i-a kauli ya kutendeka
iii. Kuamuru
kwa mfano; kachez-e!, nip-e!
iv. Kukanusha
Hapik-i, Hachez-i
v. Kuonesha wakati
kwa mfano; Aimba-po, afikapo
vi. Kuonesha mahali
kwa mfano; Aingiamo, wachezeapo
vii. Kuuliza
kwa mfano; mwatendani?mwafanyani?
viii. Virejeshi.
Kwa mfano; Amsomeaye, waandikao, kirarukacho