VIARUDHI/ VIPAMBASAUTI

 Hizi ni sifa ambazo huambatishwa katika vitamkwa na kuleta maana. Sifa hizi huambatana na vitamkwa asilia kama vile: silabi, neon, kirai na sentensi (vipashio ambavyo ni vikubwa kuliko foni na vinatumika katika mfumo wa lugha). Viarudhi hujumuisha jiografia ya mzungumzaji.

â–ºKIIMBO

Ni upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti katika usemaji. Kutokana na kiimbo tunaweza kumtambua mzungumzaji kama anauliza swali, ombi, amri, maelezo, kejeli au mshangao.

AINA ZA VIIMBO

(i)                 Kiimbo cha maelezo kwa mfano, Mtoto anakula

(ii)               Kiimbo cha kuuliza kwa mfano, Mtoto anakula?

(iii)             Kiimbo cha kuamuru kwa mfano, Nenda nje

(iv)             Kiimbo cha mshangao kwa mfano, khaa! Mtoto anakula

(v)               Kiimbo cha kejeli, Mtoto anakula

hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top