Japo Kiswahili kilikuwa kimeenea katika mataifa mengi Afrika Mashariki wakati wa ukoloni, lugha hii iliweza kukumbwa na vikwazo kadhaa ambavyo vilitatiza maenezi yake, vikwazo hivi vilitatiza kusambaa zaidi Afrika.kusingekua na vikwazo hivi Kiswahili kungekuwa lugha
ya mataifa mengi ya bara la Afrika, miongoni mwa vikwazo vilivyo kumba lugha hii ni:
1- Dharau za Wazungu kwa Waafrika
Mfumo wa utawala wa Wazungu na Waingereza, ulileta pingamizi kubwa katika maenezi ya Kiswahili. Waingereza waliwadharau sana Waafrika na mambo yao yote kwa jumla kukiwemo lugha zao. Kiswahili kama mojawapo ya Lugha za Kiafrika haingeweza kuepuka dharau hizo.
Kwa upande mwengine Wakoloni walichukulia kuwa lugha yao ya Kiengreza ilikua adhimu na yenye manufaa kuliko lugha yeyote, na yeyote aliyetaka ustaarabu lazima ajifunze Kiingereza, waliweza kukuza lumbikizo hizo kwa kupitia mashule walioanzisha na nafasi za kazi ambazo waliwapa kipawa mbele wanaojuwa Kiingereza, pia waliweka mawazo kwenye akili za watu kuwa Kiswahili hakitoshi kunfanya mtu astaarabike.
Kwa sababu hizo za chuki Waaingereza walianzisha lugha rasmi za matumizi kwa Mwafrika, hivyo basi Kiingereza kikapewa hadhi kubwa na ya juu kufanywa lugha rasmi kisha Kiswahili. Hapo basi Kiingereza kikawa ndio lugha ya Ustaarabu na yeyote aliyetaka kustaarabika alijifunza Kiingereza. Kuna fikra mbaya zaidi iliyoenezwa na Wazungu hao, nayo ni kuwa Kiswahili Hakikuwa na misamiati yakuendesha shughuli za kielimu na taaluma isipokuwa Kiingereza kwa maoni yao waliwaona Waafrika kwa watu washenzi na washamba.
Mawazo haya yaaliwaathiri sana wenyeji na wengi wakaanza kutoroka Tamaduni za kiafrika na hata lugha, na wengi wakaanza kutafuta ustaarabu katika lugha za kigeni. Kwa mfano Kenya na Uganda, kuna baadhi ya viongozi hadi leo waamini kuwa kiingreza ni bora kuliko Kiswahili na lugha nyengine za Afrika.
2- Kiswahili ni lugha geni.
Kuna baadhi ya watu walidai kuwa Kiswahili ni lugha geni yaani ni Kiarabu, nahivyo basi kilikuwa hakina nafasi hapa Africa Mashariki na yakati. Hivyo basi wakaonelea ni heri wajifunze lugha za kienyeji badali ya Kiarabu, tume ya Philips stoke ya 1924x ambayo iliteuliwa kuchunguza na kupendekeza matumiza ya lugha, nchini Kenya ilipendekeza matumizi ya lugha ya Kikamba, Kijaluo, Kikikuyu, na Kiluhya, nchini Uganda walipendekeza Kiingereza na Luganda,katika maeneo ya kifalme na hata maeneo yasiokuwa ya kimalme, nchini Zaire Waluba, Wakongo na Walingala walikataa katakata kusanifishwa kwa Kiswahili cha Kiungwana kwa sababu walidai kuwa ni lugha geni ya Afrika Mashariki na basi haina nafasi Zaire ndiposa Kifaransa kikaendelezwa na Wabelgiji.
3- Dhana kwamba Kiswahili kiliendeleza Uislamu.
Nao Wamishonari hawakukipenda Kiswahili kwa sababu kiswahili kilinasibishwa na uislamu kwa madai yakuwa Kiswahili kiliendleza Uislamu ilihali wao walitaka kuendeleza Ukiristo, hali hiyo iliwapelekea kukusanifisha Kiswahili wakidai kuwa walikuwa wakiondoa Uarabu na Uislamu katika Kiswahili, pia walidai walitaka kukipa chombo cha kueneza dini ya Ukiristi nidhamu, haya yote yalifanywa na Wameshinari wakishirikiana na Wazungu kwa kutambua hakuna lugha nyengine yaweza tumiwa kwa mambo ya Mungu isipokuwa Kiswahili.Kwa mtazamo wa makini twaweza sema lau Wakoloni na Wamishonari wangekuwa na lugha mbadala kuliko Kiswahili basi wangetumia lugha hiyo na wangeiacha lugha ya Kiswahili, lakini kwa kuwa ingekuwa gharama kufasiri baadhi ya vitabu vyao kama Biblia katika lugha nyengine za Kiafrika basi
waliazimia kutumia Kiswahili, nchini Uganda na Kenya kuna tume ziliochaguliwa
kuchunguza matumizi ya Kiswahili kwakuwa lugha hii iilihusishwa na usambazaji wa Uislamu.
4- Biashara.
Kwa jumla biashara ni miongoni mwa viekezo vikuu vilivyoifanya lugha ya Kiswahili kuenea Afrika Mashariki, ingawa hivyo biashara hii ilitumiwa na Wakoloni kuifanya lugha ya Kiswahili kuchukiwa na kuonekana lugha mbaya. Waingereza walieneza propaganda kuwa Kiswahili na wanaotumia Kiswahili wamefungamana na biashara ya watumwa, nayo fikira ikaenea kwa jamii kwani biashara ya watumwa ilikuwa ni biashara mbaya na yeyote aliyetoka maeneo ya
bara alimchukia mwenye kufanya biashara hiyo nakumuona adui, kwa hivyo Kiswahili kikachukiwa na Waswahili wenyewe wakachukiwa kwa kuhusishwa na biashara ambazo hazikuwa za kweli. Kawaida biashara siku zote huhusishwa na porojo na ukora na ujanja mwingi, basi ikawa lugha ya Kiswahili ni lugha ya wakora na wajanja wenye kufanya biashra za
watumwa, kwa sababu hizo lugha hii ikawa wengi katika wageni hasa wasiotoka maeneo ya mwambao waichukie.