Ni vipengele ambavyo hushirikiana ili kujenga lugha.kuna aina nne kuu ya vipashio ambavyo hujenga lugha, navyo ni:
1 Sauti
2 silabi
3 Neno
4 Sentensi
Katika ngazi ya chini zaidi katika vipashio hivyo huwa ni sauti ,nazo sauti huungana kujenga silabi ,silabi huunda neno na maneno huungana kujenga kipashio kikubwa zaidi ambacho ni sentensi.Vipashio hivi ndivyo nguzo ya lugha na vinapoungana ndipo lugha hujengeka.