Virai ni Vikundi vya maneno vitumiwavyo na binadamu visivyo na maana kamili. Virai huwa ni tungo zinazoundwa kwa maneno aghalabu mawili au zaidi yanayoashiria kitu kimoja na yanayojengwa juu ya neno kuu.

kirai kinaweza fasiriwa kuwa ni kipashio kidogo cha kimuundo chenye neno moja au zaidi ambacho hakina muundo wa kiima (K) na kiarifu (A). Kirai huwa na neno kuu moja linalotawala. Neno hilo linalotawala ndilo huwa aina ya kirai.

Uainishaji wa virai

Uanishaji wa virai umejikita katika aina za maneno, yaani, aina za virai zinatokana na aina za maneno. Kwa kutumia kigezo hicho tunapata aina za virai zifuatazo:

(i) Kirai nomino (KN) (ii) Kirai kivumishi (KV) (iii) Kirai kitenzi (KT) (iv) Kirai kielezi (KE) (v) Kirai kiunganishi (KU) (vi) Kirai kihisishi (KH)

(i) Kirai nomino (KN)

Hili ni kundi la maneno ambalo hutawaliwa na nomino. Kirai nomino huundwa na maneno yafuatayo:-

o   Nomino pekee. Mfano; Asha anapika, Nyangoye anaimba, Nyegera anacheza (N)

o   Nomino mbili au zaidi zinazounganishwa. Mfano; Mhindi na Sagati wanacheza. (N+U+N)

o   Nomino na kivumishi. Mfano; Mtoto mnene amekuja, Mzee mfupi ameondoka. (N+V)

o   Kiwakilishi pekee. Mfano; Yule ameondoka, Wewe umenena, Wale waliokuja. (W)

o   Kiwakilishi na kivumishi. Mfano; Yule mvivu amerudi, Wewe mlemavu njoo. (W+V)

o   Nomino na kitenzi jina. Mfano; Mchezo wa kusisimua, Wimbo wa kupendeza. (N+Ktj)

o   Nomino na kishazi tegemezi kivumishi. Mfano; Mjukuu aliyepotea, Mheshimiwa aliyeondoka. (N+βV)

(ii) Kirai kivumishi (KV)

Hiki ni kirai ambacho muundo wake umejikita katika kivumishi na maneno yanayohusiana na kivumishi katika tungo hiyo. Virai hivi kwa kawaida hujibainisha zaidi kimuundo kama sehemu ya virai nomino. Virai hivi huundwa na:-

o   Kivumishi na Kirai nomino. Mfano; Mwenye mali nyingi, Wenye watoto wengi.

o   Kivumishi na kielezi. Mfano; Mzuri sana, Mweupe pee!,Mweusi tii!, Mbaya sana.

o   Kivumishi na kirai kitenzi. Mfano; Mwenye kupiga gitaa, Mwenye kupenda sana.

o   Kivumishi na kirai kiunganishi. Mfano; Nzuri ya kupendeza, Mpungufu wa akili.

(iii) Kirai kitenzi (KT)

Kwa kuangalia muundo wa Kirai hiki huundwa kwa vitenzi vya aina zote

Vipashio vinavyounda Kirai Kitenzi

o   Kitenzi peke yake – tutapigana, nitakuja, amesimama

o   Kitenzi na nomino moja –  amempiga Juma

o   Kitenzi na nomino mbili – amempa mtoto chakula

o   Kitenzi na kitenzi – anapenda kusoma

o   Kitenzi na nomino na kitenzi – anamfundisha mtoto kusoma

o   Kitenzi, kiunganishi tegemezi na sentensi

                     amesema kwamba atarudi kesho.

o   Kitenzi, nomino, kiunganishi tegemezi na sentensi

               Amemwambia Juma kwamba atarudi mapema

(iv) Kirai kielezi (KE)

Tofauti na aina nyingine ya virai, miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi ) na neno au fungu la maneno linaloandamana nalo. Badala yake miuundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika Lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo. Zaidi kirai kielezi huelezea namna, wakati, mahali na kinachofanya tendo hilo litendeke. Mfano; Mara nyingi, Sana sana, Polepole, Jana asubuhi, Kesho mchana, n.k.

(v) Kirai kiunganishi (KU)

Kirai hiki huundwa kwa kutumia viunganishi mbalimbali. Mfano:

Ingawa

Na

Kwa kuwa

Bila

Pasipo

Sembuse

Lakini, n.k.

(vi) Kirai kihisishi (KH)

Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya vihusishikwa, na, katika,au kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno menginekirai hicho ni kile ambacho neno kuu ni kihusishi. Virai vihusishi japokuwa muundo wake hufanana ila hutofautiana kimaana, zipo maana tatu ambazo ni:-

a)  Pahala – kwa baba, katika kabati, kwenye lindo

b)  Utumizi – Kwa kisu, Kwa mkono

c)  Uhusika – Na Mjomba, Na Bibi.

Vilevile kirai kihusishi hutumiwa kutekeleza majukumu yafuatayo katika sentensi:-

ü  Kama kivumishi. Mfano; Penseli ya mjomba, Mkoba wa mama, Koti la babu

ü  Kama kielezi. Mfano; Tulisikiliza kwa makini, Tuliimba kwa shangwe, Tulisoma kwa juhudi

ü  Kama kiwakilishi. Mfano; La mjomba limetupwa, Ya shangazi imeuzwa, Wa nne ameondoka

        Zoezi

       Bainisha virai katika sentensi ifuatayo

  1. Mzazi na watoto wawili werevu sana waliwasili shuleni leo asubuhi kabla ya mwalimu. 
  2. Unaweza kuamua kunyamaza au kujitetea.