Sauti za Lugha

Sauti ni mlio unaoababishwa na mgusano au kukaribiana kwa ala za kutamkia.

Sauti pia inaweza fasiriwa kuwa ni sehemu ndogo kabisa ya neno ambayo haiwezi kugawika zaidi. Sauti nyingi huwa ni herufi moja ya alfabeti kama vile (a,e,i, b, d) ingawa pia kunazo sauti zinazoundwa kwa kuungunisha herufi mbili au zaidi (kama vile ng, nd, mb).

lugha ya kiswahili ina idadi maalumu ya sauti. sauti hizi ndizo hutumiwa kuundia maneno ya kiswahili. sauti hizi huitwa fonimu. 

 Ala za Sauti

Ni viungo vya mwili vinavyofanya kazi ya utoaji wa sauti.ala hizi ni kama vile; mapafu,koo,kaa gumu,kaka laini, n.k. ala hizi zimegawika katika kakundi mamwili makuu:

a)Ala sogezi

b) Ala tuli

Kuna makundi mawili ya sauti za lugha:

  1. Irabu

Sauti ambazo hutamkwa kwa ulaini bila hewa kuzuiliwa katika ala za sauti.

  1. Konsonanti

Sauti ambazo wakati wa kutamkwa hewa huzuiliwa katika ala za sauti

Leave a Reply

scroll to top