Silabi

Silabi ni tamko moja katika neno/herufi moja au zaidi ambazo hutamkwa pamoja.

Silabi pia inaweza fasiriwa kuwa ni kipashio cha lugha kinachotamkika, au  silabi ni mapigo ya sauti katika neno.  kwa mfano neno Kalamu lina silabi tatu, nazo ni Ka-la-mu.

jedwali hili linaonyesha mifano zaidi ya silabi katika maneno mbalimbali:

NenoSilabiIdadi ya silabi
Aliondokaa-li-o-ndo-ka5
Kalamuka-la-mu3
hufikiriihu-fi-ki-ri-i5
anasomaa-na-so-ma4

  Aina za silabi

Silabi wazi/huru

Hizi ni silabi zinazoishia kwa vokali. Nyingi kati ya silabi hizi ni zenye asili ya Kibantu. 

Mathalan:

ba/ba = baba 

sha/nga/zi = shangazi 

Silabi funge

Hizi ni silabi zinazoishia kwa konsonanti. Aghalabu asili ya silabi hizi ni lugha za kigeni. 

    Ghalibu, silabi hizi hujitokeza sehemu ya kati ya neno. 

    Mathalan :

    /lab/ da = labda 

    /il/ hali = ilhali 

    /daf/ tari = daftari 

    /dik/ teta = dikteta. 

    Miundo ya Silabi za Kiswahili

    i. silabi ya irabu pekee

    oa    o-a

    ua    u-a

    ii. silabi za konsonanti na irabu

    Soma  so-ma

    iii. silabi za konsonanti mbili na irabu / Silabi ambatano

     Silabi hizi hujumuisha consonanti mbili kisha irabu Kwa mfano mwa-mba , mwa-li-mu

    o-ndo-ka

    iv. silabi za konsonanti tatu na irabu  / Silabi changamano

    Hujumuisha konsonanti tatu na irabu moja  kwa mfano mbwe- ha

    v. silabi za konsonanti pekee

    Mchicha   m-chi-cha

    Kelbu

    Kuran

    vi. Silabi za irabu na konsonanti

    ah!,

    vii. Silabi za konsonanti, irabu na konsonanti

            Zoezi

    1. Ukitoa mifano, fafanua miundo miwili ya silabi za Kiswahili.
    2. Tenganisha silabi katika maneno yafuatayo:
      1. inkisari 
      2. baiskeli. 

    Leave a Reply

    scroll to top